Pages

Subscribe:

Friday, December 18, 2015

AY AMSHIRIKISHA DIAMOND KWENYE RMX YA ZIGO

Kwenye Post aliyoweka Ay akimpongeza Diamond kwa ushindi wa Tuzo za MTV EMA na kuahidi kuwa vitu vikubwa vinakuja basi inaonekana Rmx ya Hitsong yake ya ‘Zigo’ ni moja ya vitu hivyo vikubwa.
 
Japo mwenyewe bado hajatangaza lakini kampuni inayotengeneza video ya wimbo huo, Kampuni ya Studio Space Pictures ya Afrika Kusini imeshea picha Instagram ya wawili hao wakiwa kwenye...
utengenezaji wa video hiyo
Ay
“Earlier today with @aytanzania @ @diamondplatnumz #ZigoRemix #studiospacepictures.”

Haijulikani kama ni Diamond pekee ndiye aliyemo kwenye remix hiyo lakini kuna uwezekano mkubwa wasanii wengine wakali wakawa wameshirikishwa, AY aliwahi kusema kuwa aliwahi kumtumia Wizkid wimbo huo na alikua anataka wafanye Rmx.
Hii itakuwa mara ya pili Diamond na AY kukutana kwenye kazi ya pamoja. Diamond amewahi kuweka ladha kwenye wimbo wa AY ‘Asante.’

0 comments:

Post a Comment