Pages

Subscribe:

Thursday, December 31, 2015

ROMA: MFUMO WA ULIPAJI MIRAHABA UNAENDA KUTUINGIZA KWENYE VITA



12105229_1668899886720358_1089964568_n
Roma anahisi mfumo wa vyombo vya habari kulipa mirahaba kutokana na uchezaji kazi za wasanii utakaoanza January utachimba kaburi kwa muziki wa Tanzania.


Tunaingia katika vita ambayo tutawapoteza wapiganaji wetu wengi sana mahiri na wale watakaosalimika ni wachache sana!! Na sio kama watasalimika kwakuwa wanajua saaaana kupigana au wanazijua mbinu za kivita No. Ni kwakuwa tu walipewa...
silaha zote za kujilinda na kupambana!! 

Na hawa mahiri waliingia vitani wao kama wao na Mungu wao bila kupewa silaha yoyote ile!! 

RADIO/TV PROMOTION
Radios/Television watakuwa wanatumia vigezo gani kuchagua kuwa hii bidhaa tuinunue na hii tusiinunue? Ilhali hadi sasa hizo bidhaa zipo tu mtaani zimezagaa tena nyiiingiii saaana za kila ainaaa na za kila ladha na zinapatikana Bureeee!!! Na Wakati Mwingine Radio/Tv Station Inachukua Bidhaa hizo kwa Interest Zao Pasi hata Wadau kujua kuwa iliyochukuliwa ni nzuri sana kuliko zingine au iliyoachwa ndiyo ingeuza zaidi sokoni!! Na hadi inafkiaga wakati RADIO/TV zinakataa kuzichukua bidhaa hizo!! Na inaweza ikachukua lakini ikazitumia kwa siku chache tu na kukimbilia bidhaa nyingine!!

Hivi, tuwaze tu kimaskini hapa Ni nani akisikia swala au neno KULIPWA/MALIPO/MTALIPWA Ni nani Atachomoa!!? Nani anakataa pesa!!? Lakini unahisi kwanini katika hili wapo watu wengi tu WANASITA!? Nani anasita mbele ya pesa!!? Ni kwasababu KUNAYO NAMNA tu Hapa!! Kwani tungeambiwa Jamani kuanzia January Mkifanya SHOW Popote Pale Mnalipwa Kwanza na Taasisi flani!! Kisha ndio promota anakulipa pia!! Nani angebisha? Sana sana Swali la kwanza lingekuwa WANATOA NGAPI!!? hakuna asietaka hela!! Ila inakuja kwa njia gani!!??

Miongoni mwa vilio vikubwa vya wasanii wengi hasa WACHANGA na hasa hasa WAKONGWE ni PROMOTION!!!
Wasanii tunalilia promotions wakati mwingine TUNALIPIA kabisa ili tutangaze bidhaa zetu(nyimbo)na hili tu lilikuwa gumu sana hadi kupelekea wasanii kupotea kwenye ramani/ wengine kuwa na uhasama na vituo vya tv/radio au watangazaji/djs…. wengine kuwa frustrated na hili hadi kumess up na mashabiki!! Na mifano mingine mingi mibaya!! Haya yote yalitokea pindi msanii anapoikosa Promotion!!
Wapo wasanii walipotea kwa kipindi na wakaweza kurudi vizuri hadi sasa hivi ni vinara na wanafanya vema!!na Wameajiri vijana wengi kupitia kurudi kwao!! unadhani kwanini!!?? Ni PROMOTION tu imewarudisha ambayo ni nzuri sana! Je wapo wangapi ambao wana ndoto za kurudi!!? Na Inawezekana!! Je mnataka Ndoto zao zisitimie tena!!?

Unadhani Radio/Tv station kwa sasa zinaweza zitaamua kupromote kumrudisha msanii tena kwa kumlipa wao kama radio!? Yaani mtu yupo nyumbani kwake hasikiki tena….alishatoa ngoma tatu mfululizo zimekataa kisha tumfate tumwambie sasa tunakulipa toka kwako twende ukafanye kazi!!?Tunakupromote na tunakulipa!!Si atasema ZALI LA MTENDE Hili!! Itawezekana kweli?

AU NDIO INAKUWA ILE YA ALIEPOTEA NDIO KASHAPOTEA HARUDI TENA!!? Ambayo haitakiwi kuna watu wana vipaji kwa Sanaa yetu ilivo wanahitaji sana nafasi za pili pasipo Mipaka kama hii tunayotaka kuwawekea!!
Sasa leo ikiwekwa kuwa Television/Radio Ikipiga kazi ya Msanii Imlipe!! Msanii yule yule ambae mimi tu kama Radio Ananililiaga nimpigie Bure na Sipigi!!Leo NIMLIPE!!? Sawa pesa za kulipwa wasanii zipo/Sheria inaruhusu pia!! Tatizo Radio/Tv station WAPO TAYARI!!? Kwa sasa!!? Na Je Radio zote hadi Hasa hizi Local za mikoani!!?
Ambazo zipo nyingi sana na Kila siku zinalalamika Hazipati MATANGAZO!
Local Radio nyingi zinashindwa kuwalipa Mishahara wafanyakazi wao/ watangazaji/Madjs kwasababu wanalalamika Radio Haiwaingizii Pesa kupitia matangazo!! Je Wataweza kuendesha radio na kulipa Wasanii!!???

TUZO
Kutakuwa na sheria za kuzitaka radio zinunue kazi za wasanii wote bila interest zao kama radio. Maana Kama radio inaamua Inunue Ngoma za Stamina Na Kala tu na kuzipromote hizo hizo kisha ikaja tuzo za KILLI MUSIC je hao wasanii wawili tu ndio watakuwa wanashindana katika ubora kwa Mwaka huo!!?? Huoni kama tumeziba Mianya ya wengine wengi wenye vipaji kwasababu tulishawawekea mipaka Awali kutokana na Interest za Kibiashara!!? Sio kama huu mfumo utaathiri mambo mengi sana!!??

HIP HOP
Katika Tasnia Ya Hip Hop pengine tokea atoke MSODOKI Takribani miaka mitatu/miwili iliyopita, nahisi hatujapata zao lingine ambalo Limefikia nafasi aliyokuwepo Msodoki!!! Tofauti na huku kwa wenzetu wanaoimba tunaweza ona kuna mazao mengi kila siku!!
Haina maana kuwa hakuna vijana wanaofanya vizuri katika HIPHOP hapana, wapo wazuri sana lakini hawapati tu ile perfect PROMOTION!! Hilo ni Tatizo!! Muziki wa HipHop sidhani kama unapewa asilimia kubwa sana kwenye Promotions. Na sio sawa eti tuwe confortable kwasababu tu tunao wasanii watano tu wa HipHop ktk Mainstream!!

FINALLY
Wapo wasanii ambao watakuwa confortable kwasasa na hii situation na ni kwasababu tu Wana Silaha hivyo wanajiamini watashinda vita!!
Ni wazo zuri sana lilikuwa na ipo siku tutalihitaji katika soko letu lakini sio leo, ni kama alieleta wazo hili ametukurupusha!! Kuna hasara nyingi kuliko faida tutakayopata!! Hata hiyo pesa tutakayopata kwa mwaka kimakadirio ni ndogo sana tofauti na ukitoa wimbo kisha ukafanyiwa promotions nzuri ukawa Hit kisha ukafanya Shows!! Otherwise tunaenda kuua shows za pesa nyingi kwa pesa ndogo za mirabaha!!
Watazameni na wale ambao hawana silaha…wengine ndio wametoka depo juzi tu hata hawajaiva…mkiwaingiza katika hii vita ni kuwajengea makaburi mapema!!!

MAONI
Tuzibe gaps zingine kwanza katika sanaa yetu(zipo nyingi na kuna vingi vya kurekebisha kabla hatujaanza na hili)Ni jambo Jema kabisa hili lakini sio kwa hatua ya sanaa yetu ilipo sasa, tuanze na mengine!! kisha tukishajiimarisha wote na silaha tukawa nazo wote basi utakuwa ni muda wetu kuingia vitani!! Na tutashinda wote na
TUTASHANGILIA USHINDI WOTE!!

0 comments:

Post a Comment