Pages

Subscribe:

Tuesday, December 29, 2015

CYRILL NDIYE ALIYE MFANYA JUX AACHE KURAP

12112282_968978856493247_182766289650621399_n


Cyrill Kamikaze amesema yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa ya kumbadilisha member mwenzake wa kundi la Wakacha, Jux kuacha kurap na kuanza kuimba.
 

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Cyrill alisema hatua hiyo ndiyo ilimfanya Jux aendelee kufanya vizuri zaidi “Mimi ndiye nilimforce sana Jux kuingia kwenye muziki, yaani alikuwa ni mwanangu na ni ndugu yangu. Alikuwa anarap, nikamwambia ‘wewe...
unaweza kuimba’ nikamwelekeza halafu nikampeleka studio akanifanyia chorus ya wimbo wangu wa kwanza,” alisema.
“Kwahiyo ukiachana na hayo yote sisi ni watu tuliokuwa kama mapacha fulani hivi, ukiachana na muziki mimi na Jux tulikuwa washkaji zaidi.” 

Pia Cyrill amesema kundi la Wakacha linaloundwa na yeye, Jux pamoja Gigga Flow linatarajia kurudi mapema mwakani.

0 comments:

Post a Comment