Pages

Subscribe:

Thursday, December 31, 2015

CHEGE AANZA KUINUSA MTV BASE NA NGOMA YA SWEETY SWEETY



chege nw
Ni ndoto za kila msanii anayewekeza pesa zake kwenda kufanya video nje ya nchi na waongozaji wa nje kuona video yake inampigisha hatua moja mbele, moja wapo ikiwa ni kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya nje.


Chege ni miongoni mwa wasanii walioachia video mpya hivi karibuni, na video yake ya ‘Sweety Sweety’ iliyoongozwa na Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films baada ya kupata airplay kwenye kituo cha MTV Base kwa...
siku 12 imeanza kunusa chati ya nyimbo bora za Afrika za kituo hicho wiki hii kwa kuingia kama ‘Bonus’.

 chege bonus

“HATIMAE ILE NGOMA YENU PENDWA #sweetysweety BAADA YA SIKU 12 TU,IMEINGIZWA KWENYE BONUNS TRACK KTK CHAT ZA AFRICA,ahsante sana sana sana @mtvbaseafrica ……..finally your beloved song SweetySweety after only 12 days has entered as a bonus track for African chat..thank you very very much @mtvbaseafrica.” Aliandika Chege Instagram.

0 comments:

Post a Comment