Pages

Subscribe:

Tuesday, December 29, 2015

NAY WA MITEGO AFUNGUKA KUHUSU MWANAMKE ATAKAYE MUOA

Chagga-na-Nay


Nay Wa Mitego ni staa ambaye miezi michache iliyopita alikuwa hakosekani kwenye ‘headlines’ kutokana na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa Bongo movie, Shamsa Ford uliokuwa ukifatiliwa sana na mashabiki wao.


Uhusiano wa Nay na Shamsa ambao kwa mujibu wa Nay ulidumu kwa takribani miezi mitano, ulizaliwa muda mfupi baada ya...
Nay kuachana na mama wa mtoto wake wa tatu Curtis, Siwema ambaye baada ya kujifungua mtoto huyo waliachana na Nay kumchukua mwanaye.


Siku chache zilizopita Nay ameonekana ameanzisha ukaribu na ex wa Prezzo, mrembo Mtanzania aitwaye Chagga Barbie aishiye Marekani, ambaye Nay amekiri kuwa wanapendana licha ya kusita kuweka wazi kama watambulike kama couple, huenda labda kwa sababu bado hawajawahi kuonana ana kwa ana.

Akihojiwa na Millard Ayo, Nay ambaye ni baba wa watoto watatu wenye mama tofauti alipoulizwa kuhusu lini na ni mwanamke gani anayefikiria kuja kumuoa, hili ndio jibu lake: “Mama wa mtoto wangu wa nne, maybe anaweza akaja kuwa ndio mke wangu” alisema Nay.

0 comments:

Post a Comment