Pages

Subscribe:

Wednesday, January 28, 2015

CLUB OLYMPIA JIJINI DAR YAWAKA MOTO

CLUB Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema. Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema... moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto. Aliongeza kwamba zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.

0 comments:

Post a Comment