Pages

Subscribe:

Thursday, January 22, 2015

MADEE: HAO MA-MISS WAZEE KAMA VIPI MWAKA KESHO NAMLETA BIBI YANGU AGOMBEE

Wimbo mpya wa Madee ‘Vuvula’ haukuishia kumchana Chidi Benz peke yake(Ingia hapa) , upo mstari mwingine ambao unamlenga Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga Mstari huo unasema: “Hey Anko Lunde, hao... Mamiss wazee kama vipi mwaka kesho namleta bibi yangu agombee.” “Kuna tatizo lilitokea lilipita kuhusu mamiss nini, so nimejaribu kumwelewesha tu ambaye ni Vuvula ajaribu kuwa makini baadae akiwa anasajili mamiss wake”. Alisema Madee alipokuwa akielezea maana ya wimbo wake. Madee aliwahi kusema kupitia moja ya vituo vya radio kuwa maana ya Vuvula ni “mtu mshamba ambaye hajielewi.”

0 comments:

Post a Comment