Pages

Subscribe:

Friday, January 30, 2015

MIMBA YA AUNTY EZEKIEL YAWA FARAJA KUBWA KWA IYOBO

Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul  ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa filamu, Aunty  Ezekiel.
Akizungumzia ujauzito wa mpenzi wake,  Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema... kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.

“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

0 comments:

Post a Comment