Pages

Subscribe:

Monday, January 26, 2015

NIKKI MBISHI AWATOLEA UVIVU MDUNDO NA WASANII WA BONGO

Rapper alietangaza kuacha Muziki siku chache za nyuma Nikki Zohan (Baba Malcom) sasa ameamua kuwatolea uvivu na kuwachana Wasanii na Site ya Mdundo ambayo inahusika na kuuza nyimbo.
Nikki ameonekana akilalamika kuwa amekuwa akidai malipo yake bila kupata mafanikio yoyote yale na kudai kuwa walipokuwa wanamtafuta walionesha ushirikiano lakini kwa sasa... maana pesa imeshaingia ushirikiano ule umepotea, pia kwa taarifa aliyotoa kuwa yeye ndio msanii alieongoza kwa Download nyingi zaidi East Africa kwenye mtandao huo wa Mdundo.
Rapper huyo ameonekana kuchukizwa sana na utaratibu / huduma za wadai wake hao mpaka kufikia hatua ya kuwatukana kupitia Acc yake ya Twitter.

0 comments:

Post a Comment