Pages

Subscribe:

Saturday, January 24, 2015

JUX AELEZA UKWELI JUU YA UHUSIANO WAKE NA VANESSA MDEE

NI fununu tu! Mwanamuziki wa kizazi kipya, Juma Jux, ameweka bayana kile kinachoendelea kati yake na Vanessa Mdee ‘V Money’ kuwa ni mambo ya kikazi na si uhusiano wa kimapenzi. Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV Online, Jux aliyasema hayo kutokana na tetesi zilizokuwa zikiandikwa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba amejiweka kwa mwanadada huyo anayetamba na... Wimbo wa Siri alioshirikiana na Barnaba.

“Ni fununu tu, hakuna jingine. Mimi na Vanessa tupo kikazi, nakumbuka nilipokuwa nataka kufanya video yangu ya Sisikii, nilikuwa natafuta msichana wa kuwa naye kwenye video, kwa sababu alikuwepo, basi hakukuwa na jinsi, nikaamua kumtumia kwani aliujua wimbo vizuri hivyo nikaamini kwamba video ingekuwa poa sana na kweli ikawa hivyo,” alisema Jux.

0 comments:

Post a Comment