Pages

Subscribe:

Thursday, January 22, 2015

KOLETA: SASA NIPO TAYARI KUZAA BILA NDOA

Kweli ujana ni maji ya moto: Kutokana na umri kumtupa mkono, mwigizaji wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ ameibuka na kutengua kauli aliyowahi kuitoa kwamba hawezi kuzaa nje ya ndoa na kusema kwa sasa yupo tayari kufanya hivyo muda wowote. Akizungumza na mwandishi, Koleta alisema... kwa sasa yupo tayari kuzaa hata bila ndoa kwani ni muda mrefu amekuwa akitamani kuitwa mama na amesubiri ndoa bila mafanikio. “Umri unakwenda nami nahitaji kuitwa mama hivyo nikipata ujauzito nazaa kwani cha muhimu zaidi ni mtoto halafu kama Mungu amenipangia kuwa na ndoa itakuja baadaye,” alisema Koleta

0 comments:

Post a Comment