Pages

Subscribe:

Wednesday, January 21, 2015

MATAPELI WAICHAFUA IKULU YA TANZANIA

Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam nchini Tanzania imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao ni matapeli na wanatumia vibaya jina la ikulu kwa kusema kwamba kuna nafasi za ajira na wana uwezo wa... kuwapatia ajira kwa kutoa fedha. Tahadhari hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kutokea kwa matukio kadhaa ya mfululizo ya watu kutapeliwa kwa kutafutiwa kazi ikulu.

0 comments:

Post a Comment