Pages

Subscribe:

Tuesday, July 26, 2016

VANESSA MDEE NA JUX WAFIKIA HOTEL YA SH. MIL6.4 KWA SIKU KWENYE MAPUMZIKO YAO

Vanessa Mdee na mpenzi wake Jux wameamua kwenda kupumzika kwa muda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Wawili hao wamelazimika kusimamisha ratiba zao ndefu za muziki na biashara kujionea maajabu kwenye mbuga hiyo maarufu duniani iliyopo wilayani Serengeti, mkoani Mara.

Wamefikia kwenye moja ya hoteli za mbugani bora zaidi duniani, Singita Serengeti Grumeti. Hoteli hizo zinazomilikiwa na wawekezaji wa Afrika Kusini, ni miongoni mwa hoteli zinazotoza gharama kubwa zaidi kwenye... mbuga za wanyama barani Afrika.

Wawili hao wamefikia kwenye hoteli ya Faru Faru Lodge ambayo ni miongoni wa himaya za Singita zilizo katikati kabisa mwa mbuga hiyo kiasi ambacho wakati mwingine wageni huwezi kuwaona wanyama wakiwa wamejipumzisha kwenye vyumba vyao.

Kwa mujibu wa gharama za mwaka 2016 za kulala Faru Faru Lodge, katika kipindi hiki kinachojulikana kwa lugha za mbugani kama ‘high season’ ambacho huanzia June 1 hadi Octoba 31, suite ya bei rahisi zaidi (double/twin) hutoza dola 1,500 (zaidi ya shilingi milioni 3.2) kwa mtu mzima, kwa usiki mmoja (per adult per night).


Hiyo ina maana kuwa Vanessa Mdee na Jux wanalipa shilingi milioni 6.4 kwa usiku mmoja kulala Faru Faru Lodge. Hata hivyo Jux alianza kwa kufikia Sasakwa Lodge ambayo ina gharama kubwa zaidi kuliko Faru Faru. Yenyewe bei ya chini kwa usiku mmoja kwenye high season ni dola 1995 ambazo ni takriban shilingi milioni 4.2 za Kitanzania.

Akipost picha ya Vanessa akiwa kwenye Jacuzzi, mbele kukiwa na glasi mbili za champagne, akifurahia mandhari ya mbuga hiyo, Jux ameandika: Day 1 at Sasakwa Lodge was nice but the queen arrived on day 2 so we had to upgrade for that better view Farufaru is almost as dreamy as her #Tanzania #Serengeti #Vacation.”

Naye Vee kwenye picha hiyo hiyo aliyoiweka Instagram, aliandika: Reboot in session #SheKing #OurSingita. Kwenye picha nyingine aliandika #Day 1 at Faru Faru. Much needed vacay. #Safari #Tanzania #Serengeti #Africa #UtaliiwaNdani #OurSingita.”

0 comments:

Post a Comment