Pages

Subscribe:

Wednesday, July 27, 2016

DAYNA: NAONA KAMA BAHATI KUFANYA KAZI NA MR T TOUCH

Dayna
Dayna Nyange amefafanua sababu inayomfanya afanye kazi nyingi na mtayarishaji wa muziki, Mr T-Touch kuwa ni kutokana na maelewano mazuri waliokuwa nayo. Akiongea siku ya jana muimbaji huyo alisema kuwa ni kama bahati kwake kukutana na kufanya kazi na Mr T-Touch.

“Nimeamua kumtumia Mr T-Touch kwenye nyimbo zangu tatu ikiwemo hii mpya ‘Komale’ kwa sababu ni producer ambaye nimeshafanya naye kazi zaidi ya moja na...
tunaelewana sana,” amesema Dayna.
“Namheshimu sana na namshukuru sana kwa jinsi tunavyoendelea kufanya kazi pia ni producer mkali sana. Naona ni kama bahati kufahamiana naye na kufanya kazi na yeye na tutaendelea kufanya kazi nyingi sana,” ameongeza.

Wiki iliyopita Dayna ameachia wimbo wake mpya ‘Komela’ aliomshirikisha Bill Nas na umezidi kufanya vizuri kwenye radio mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment