Pages

Subscribe:

Tuesday, July 26, 2016

RAYMOND: VIDEO YA NATAFUTA KIKI IMEKWAMISHWA NA WASANII WALIO TAJWA

Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond aka RayVanny ameitaja sababu kubwa ya kuchelewa kwa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ kuwa ni baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo huo kushindwa kuonesha ushirikiano. Muimbaji huyo amefunguka kuwa baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ wamekuwa wagumu kupatikana.
Aidha Raymond ameongeza kuwa menejimenti yake ilimleta director kutoka nje lakini baada ya baadhi ya wasanii kushindwa kuonesha ushirikiano wakamruhusu kurudi... kwao kwanza.
Kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kuiona video ya wimbo huo, Raymond ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni Guitar Version. Hata hivyo Raymond amedai video hiyo itafanyika japo hajataja itachukuwa muda gani.

0 comments:

Post a Comment