Pages

Subscribe:

Sunday, July 31, 2016

PAM D: BAADHI YA WANAUME WANATUOGOPA WASANII WA KIKE

Msanii wa kike Pam D ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'Nipe nono' ambao amemshirikisha Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa kuna baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwaogopa sana wasanii wa kike wa bongo fleva.

Amesema wanaume wengi wamekuwa wakidhani kuwa wasanii hao wanawasaliti.
Pam D amesema hayo na kudai kuwa hata yeye anatamani kumpata mtu ambaye atakuwa 'serious' katika mahusiano lakini tatizo...
kubwa lililopo ni kwamba kuna baadhi ya wanaume wamekuwa hawajiamini kutoka na wasanii wa kike wakidhani kuwa wana mambo mengi, au wanawasaliti.

"Kwanza kuna baadhi ya wanaume unakuta wanatuogopa ujue, wanaona labda tunawadanganya, sijui nini hawajiamini wenyewe" alisema Pam D
Mbali na hilo Pam D alisema kwa sasa anatamani kupata mwanaume ambaye yupo 'serious' kwenye mahusiano na kumtolea mfano Nay wa Mitego kuwa kama angekuwa na mtu kama huyo angeshukuru sana.

0 comments:

Post a Comment