Pages

Subscribe:

Monday, July 25, 2016

BABA LEVO: DIAMOND NDIYO MKOMBOZI WA SANAA YETU


diamond
Msanii wa muziki na mchekeshaji, Baba Levo ambaye sasa ni diwani wa Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma, amemsifia Diamond kuwa ni kama mkombozi wa muziki hapa Bongo lakini amekumbushia alivyowahi kukopi mistari ya wimbo wake.Kupitia akaunti yake ya Instagram, muimbaji huyo ameandika:

Tutaruka rukaaaaa lakini bado@diamondplatnumz atakuwa ndo mkombozi wa hii sanaa yetu… Kututangaza katufungulia njia katufungulia masoko ya nje ya tanzania.. Hahahahaa #SIMBA Mi najisemwa ukweli bhana MONDI ni...
NOUMA japo huko siku za nyuma asha wahi kunikwangua ka korasi kangu hahahaaaa #D_ONE
Septemba 4, mwaka 2013 Baba Levo kupitia akaunti yake ya Facebook alilalamika kwa madai kuwa Diamond amemuibia mistari ya wimbo wake ‘Sweaty Sweaty’.
“ZAMANI nilikuwa nikiskia mtu analalamika kaibiwa wimbo au kaibiwa njia. Nilikuwa naona ni kama maigizo na mtu kutafuta kick ya kupandia .ila leo nasema wazi DAIMOND PLATNUM amechukua korasi ya wimbo wangu niliopanga kufanyanae unaitwa SWEATY SWEATY na kuiimba kwenye wimbo wake mpya NO 1 .. kanizungusha sana kumbe alikuwa na lengo lake…ila baridaa maisha yanasonga…” aliandika Baba Levo.

Japo hayo yamewahi kutokea lakini Baba Levo ameonekana kumtaja mara kwa mara Diamond kama msanii anayemkubali kutokana na mafanikio aliyoyapata na kutokata tamaa japo kuna vikwanzo vingi anavipitia

0 comments:

Post a Comment