Pages

Subscribe:

Monday, July 25, 2016

DAYNA NYANGE: SIPENDI KUTOKA NA VIJANA WADOGO

post-feature-image
Msanii Dayna Nyange ambaye kwa sasa ameachia wimbo wake mpya akiwa ameshirikiana na Bill Nas amefunguka na kusema kuwa yeye kwenye mahusiano hapendi kutoka na watoto wadogo kwani watoto wadogo kwanza wanakomelea sana lakini wanakuwa na mambo mengi.

Dyana Nyange alisema hayo kuwa mara nyingi anapenda kuwa na mahusiano na watu wazima ambao wanajitambua na kujielewa, kwani watoto wa dogo wanakuwa...

wanasumbua sana kutokana na umri wao kuwaruhusu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo yeye huwakwepa.

“Unajua mimi nina wivu sana hivyo naogopa kutoka na watoto wadogo kimapenzi, lakini pia watoto wadogo wanakuwa na mambo mengi sana unakuta wewe unahitaji kufanya maisha lakini kumbe mwenzako anawaza kuwa na wewe kwa kukomelea tu, pili wanakuwa na mahusiano na watu wengi, wanawaza starehe sana na dunia yetu ya leo hii maradhi mengi, mimi nawaogopa sana vijana” alisisitiza Dyana Nyange.

Mbali na hilo msanii Dyana Nyange aliongea kwa matani huku akicheka na kusema amekuwa akiwakimbia na kuwakwepa sana vijana wadogo sababu wanakomelea sana (wanakamia sana kwenye mapenzi).

“Unakuta wewe umepanga kufanya maisha unakutana na kijana kumbe yeye bado hayupo tayari na bahati mbaya umepata ujauzito hataki si ndiyo hapo utaanza kulea mtoto peke yako, lakini pia vijana wanakomelea sana” aliongea Dyana Nyange huku akicheka.

Dyana Nyange ameachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Komela’ ambao ameshirikiana na Bill Nas.

0 comments:

Post a Comment