Pages

Subscribe:

Friday, July 29, 2016

JOH MAKINI ASHANGAZWA NA TETESI ZA KUGOMBANA NA NAHREEL


Joh
Joh Makini amesema maneno anayoyasikia mtandaoni kuwa Weusi na producer Nahreel hawana tena maelewano mazuri yanamshangaza na hajui yameanzia wapi. Tetesi hizo zimedai kuwa tangu Nahreel abadilishe utaratibu wa kurekodi kwenye studio yake ya The Industry, Weusi na wasanii wengine wa karibu nayo wameonekana...
kujitenga.

“Watu unajua mimi wananishangaza sana, nilikuwa na Nahreel juzi tulikuwa Jamaican restaurant tunapiga story. Nashangaa kwanini watu huwa wanapenda kusambaza habari ambazo sio za kujenga ni za kubomoa. Anyway unawaacha tu watu waongee lakini maisha yanaendelea,” Joh aliiambia Bongo5.

“Tuko poa na Nahreel na kazi zinapigwa kama kawaida yaani,” ameongeza. Amedai kuwa hata beat ya collabo yake na rapper wa Afrika Kusini, Khuli Chana ametayarisha Nahreel.
Wiki mbili zilizopita Jux pia alizungumzia uhusiano wake na Nahreel na kusema bado wapo karibu kama kawaida.

0 comments:

Post a Comment