Pages

Subscribe:

Sunday, July 31, 2016

MAMA DIAMOND ANYWEA BAADA YA TETESI ZA MIMBA YA ZARI KUZUKA


ZARI NA MAMA DIAMOND
Imevuja! Baada ya muda mrefu kusambaa kwa habari kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ‘haivi’ na mwandani wa msanii huyo, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’, imedaiwa kuwa kwa sasa bi mkubwa huyo amenywea kwa kumkubali Zari.

Taarifa hizo zilizopenyezwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia ya Diamond zimeeleza kuwa, hivi karibuni mama Diamond amesalimu amri na kutamka hadharani kuwa Zari ni...
kiboko kuliko wanawake wote ambao mwanaye amewahi kuwa nao.

“Mama Diamond kanywea kwa Zari na wala hana lolote la kusema, unajua Zari kamtuliza sana Diamond! Si kama alivyokuwa huko nyuma. Huwezi amini juzikati mama Diamond katamka kabisa kwamba hakuna mwanamke kama Zari maana amemtuliza Diamond vilivyo,” kilichonga chanzo hicho.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Mwana Habari alimpandia hewani mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo baada kuelezwa kila kitu bi mkubwa huyo alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Eeeh mwanangu…eee..”
Mwandishi aliendelea kumpigia simu mama Diamond baada ya kukata lakini hakuweza kupokea tena.
Zari na mama Diamond wamedaiwa kuwa katika msuguano wa chinichini kutokana na kutoelewana tabia na kila mmoja kutomzungumzia mwenzake kwa mazuri hivyo kwa mama Diamond kudaiwa kusema anamkubali mkwewe huyo, ni dhahiri kwamba amekubali yaishe!

0 comments:

Post a Comment