Pages

Subscribe:

Saturday, July 30, 2016

MUBENGA AFUNGUKA BAADA YA TETESI KUWA KADHURUMUWA NA OMMY DIMPOZ

ommy-dimpoz-na-Meneja-wake-Mubengamuba
Aliyekuwa meneja wa msanii wa muziki Ommy Dimpoz, Mubenga, amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kilicho muachanisha na Ommy Dimpoz ni kudhurumiana pesa. Hapo awali Mubenga alisema aliamua kuachana na Ommy Dimpoz ili...
na yeye afanye mambo yake bifansi pamoja na kuanzisha label yake mpya ya muziki itayokuwa inasimamia wasanii.

“Kiukweli ni kwamba hakuna tatizo, ni mambo ya kazi PKP ni kama nyumbani tu, nimeamua kuhama nyumbani na kwenda kuanzisha maisha yangu,” Mubenga alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

“Hakuna kudhurumiana, hiyo stori ndo naisikia kwako, hakuna kitu kama hicho, na mimi sina tatizo na Ommy Dimpoz,”
Mubenga kwa sasa ameanzisha label yake mpya ‘Bengaz Entertainment’ ambayo itaanza kusaini wasanii wa muziki hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment