Pages

Subscribe:

Wednesday, July 27, 2016

JAY MOE AFUNGUKA KUWA NA UHUSIANO NA SHILOLE

Mwanamuziki rapa nchini anayetikisa kwa ngoma ya 'Pesa Madafu', Jay Moe amekuwa akionekana karibu sana na rapa Bilnass ambaye anatikisa na ngoma ya 'Chafu Pozi' kitu ambacho ni njia pekee ya Jay Moe kumpata mrembo Shilole.

Baada ya kuwepo kwa tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi na zaidi kuonekana picha wako pamoja kwenye moja ya eneo za kula bata wakati wa usiku, Mwaandishi alimtafuta rapa Jay Moe. Jay alifunguka nakusema ndio... mara ya kwanza yeye kusikia habari hizo.

"Ndio kwanza nasikia mambo hayo, sijui mamneno hayo yametoka wapi, ni mambo ya muziki tu na uvumi wa stori tofauti, kama picha mimi ni msanii na kama wasanii picha ni kawaida tu ila hakuna kinachoendelea kati yangu na Shilole"
Jay Moe anatajwa kuwa karibu na Shilole kutokana na urafiki wake na Billnas.

0 comments:

Post a Comment