Pages

Subscribe:

Tuesday, July 19, 2016

JUX KUUZA VIATU VYA AFRICAN BOY KWA Tsh.200,000


13108563_570785076419832_1652219953_n
Jux amedai kuwa brand ya African Boy imegeuka kuwa kitu kinachomuingizia fedha nyingi kwa sasa. Amedai kuwa jinsi nguo zake zinavyofanya vizuri kwa sasa kumemfanya awe na mipango mikubwa zaidi siku za usoni. 

“Kwa muda mfupi African Boy imenipa pesa ambayo naweza kusema kwamba imenisaidia vitu vingi sana. Ni kitu ambacho kinafanya vizuri sana, nikileta mzigo sasa hivi in two weeks au one week hata ukiwa...
mkubwa vipi, mara nyingi sana nakuwa nimemaliza,” Jux ameiambia Bongo5.
13256692_131402337267978_416813564_n
Anasema mpango wake ni kuwa na duka kubwa litakalokuwa likiuza bidhaa zake tu. Kwa upande wa viatu vya brand yake, amedai kuwa aliletewa sample lakini hakuridhishwa na kiwango chake kwakuwa vitakuwa vikiuzwa kwa bei kubwa kidogo.

Amesema kiatu chake kitauzwa kwa shilingi laki mbili na kwamba kitakuwa na ubora wa hali ya juu.

0 comments:

Post a Comment