Pages

Subscribe:

Tuesday, July 26, 2016

OMMY DIMPOZ AACHANA NA MENEJA WAKE MUBENGA

post-feature-image
Aliyekuwa meneja wa PKP ya Ommy Dimpoz, Mubenga, amesema hafanyi tena kazi na muimbaji huyo wa wimbo ‘Achia Boby’ huku akiweka wazi mpango wa kuanzisha label yake mpya. Mubenga ambaye alifanya kazi kwa muda mrefu na Ommy Dimpoz amedai kuwa ameakua kuachana na PKP ili afanye mambo yake mengine.

Mubenga amesema “Mimi NILIKUWA nafanya kazi na kuchukua asilimia flani tu Pkp ila kwa sasa nina movement yangu kwenye kazi zangu hizi hizi, bado hatujaanza kuachia kazi ila tutatangaza...

soon” Mubenga amekuwa meneja wa kazi za sanaa za msanii Ommy Dimpoz na Nedy Music kwa muda mrefu.

“Kwa sasa najipanga ili kuja na kampuni yangu ambayo itaitwa Bangerz Entertainment ambayo itakuwa inahusika na maswala yote ya burudani, hivyo wadau wangu waelewe kwamba kwa sasa sifanyi kazi tena na pozi kwa pozi” alisema Mubenga

Hata hivyo Mubenga hakuweka wazi sababu iliyopelekea yeye kuachana na PKP huku akisisitiza kuwa anarudi katika kazi zake alizokuwa akizifanya kabla ya kuungana na pozi kwa pozi.

0 comments:

Post a Comment