Pages

Subscribe:

Friday, September 22, 2017

AFYA: SABABU TANO ZINAZO FANYA USHAULIWE KUACHA KULA SEMBE

ugali wa sembe ni upi?
huu ni ule ugali ambao unakua mweupe sana baada ya kupikwa, hii ni sababu ya kukobolewa kwa mahindi au  kuondoa sehemu ya juu kabisa ya ya mahindi na kutengeneza pumba kisha kiini cha ndani cha mahindi kutengeneza unga.

                                                               
pamoja na makundi yote ya walaji kuona wanakula ugali wa aina moja lakini sio kama wanavyofikiria kwani chakula wanachokula ni tofauti kabisa. ugali wa sembe una madhara makubwa kuliko dona kama...

ifuatavyo

ukosefu wa vitamini muhimu; 
unga wa sembe hauna vitamin b1 ambayo inapatikana kwenye ugali wa dona, vitamin hii ni muhimu sana kwa ajili ya kazi mbalimbali za mwili ikiwemo kusaidia mwili kutengeneza nguvu za mwili, kuchoma mafuta mwilini,kazi za ubongo,moyo,mishipa ya fahamu, na misuli...ukosefu wa vitamin hii husababisha kushindwa kazi kwa moyo, akili kidogo darasani, ganzi ya mwili, msongo wa mawazo na shida ya tumbo na utumbo.

kuongezeka unene;
ugali wa sembe kitaalamu uko highly viscous hali ambayo inaongeza mzigo kwa mfumo wa chakula na kusababisha watu kuongezeka lakini pia mlaji wa dona anakua anakula sehemu ya wanga na sehemu ya vitamini na madini tofauti na huyu wa sembe ambayo mlaji anakula wanga tupu na wanga ndio moja ya vyanzo vikuu vya unene.

chanzo cha magonjwa ya kisasa; 
ugali wa sembe una tindikali nyingi sana kitaalamu kama highly acidic, tindikali hii ndio chanzo cha kuharibu viungo mbalimbali vya mwili na kuleta magonjwa ya kisasa kama kisukari, magonjwa ya moyo, presha, na kansa....vyakula kama mboga za majani na matunda hua na tindikali kidogo hivyo hufanya kazi ya kuzuia magonjwa haya.

ukosefu wa madini muhimu; 
madini muhimu kama phosphorus,magnesium,zinc,calcium,manganese,zinc, na selenium ni muhimu sana kwa kazi za kimwili lakini hupatikana kwenye mahindi kabla hayajakobolewa na baada ya kukobolewa hubaki bila madini kabisa.

kiasi kidogo sana cha nyuzinyuzi; 
nyunzinyuzi au fibres kwenye chakula ni muhimu sana kwa ajili ya kusafisha utumbo, kuondoa sumu mwilini na kuzuia mtu kupata choo ngumu lakini nyunyuzi hizi hazipatikani kwenye ugali wa sembe na matokeo yake mlaji hukosa faida zote hizo kwa kupata choo ngumu, sumu mwilini na kua na mfumo wa chakula ambao sio msafi.

1 comments:

Unknown said...

Hakika ni ukweli mtupu mwenye akili yenye akili na atambue tangu sasa na kufanya maamuzi sahihi lakini wale wanaoenenda na utandawazi eti ni ukisasa haya na waendelee kula sembe zao,elimu muhimu lama hizi tunazipata bure kabisa kwa bando kidogo sana lakini hatusomi na kama tukisom hatufanyii kazi hivyo basi imefika wakati sahihi wa kubadilika,kitu kingine eti Binadamu anazidiwa akili na panya ,maana panya hata ukimwekea mahindi yaliyokobolewa katika shimo lake utayakuta ulivyoyaweka hawali kabisa yani tujifunzi kupitia viumbe hawa ambao tunajivuna ya kwamba tunawazidi akili hebu someni mithali 6:6.

Post a Comment