Pages

Subscribe:

Wednesday, September 20, 2017

SHAMSA FORD AAMUA KUMPA ZARI USHAURI BAADA YA DIAMOND KUCHEAT



Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ametia neno kile kinachoendelea kwa sasa kati ya Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Mapema jana Diamond alikiri kuwa mtoto wa Hamissa ni mwanaye licha ya kuwa katika mahusiano na Baby Mama wake, Zari The boss Lady. Katika mtandao wa Instagram Shamsa ameandika...
ujumbe mfupi na kueleza kuwa Zari anastahili pongezi kwa kujua yote na kuamua kukaa kimya.

Kiukweli anasitahili pongezi kubwa sana, najaribu kuvaa viatu vyake kama mwanamke nayaona maumivu yake. Ila pamoja na yote hakuna mwanaume asiyecheat. Zari endelea kumpenda Nassibu wako kamwe usimuache kwa ajili ya mwanamke mwenzio. NCHI YAKO IKIVAMIWA UNATAKIWA KUPAMBANA NA SI KUKIMBIA.

Ujumbe wa Shamsa ni katika post ya Steve Nyerere ambaye naye aliandika, “Wewe ni Malkia wa nguvu na yote yaliyopita bado umesimama na mmeo kuangalia watoto, Be Strong”.

0 comments:

Post a Comment