Pages

Subscribe:

Saturday, September 30, 2017

NEDY MUSIC AWATAKA WASANII WAACHANE NA MAISHA YA KUIGIZA



Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Nedy Music amesema si vizuri kwa wasanii kuishi maisha ya kuigiza. Muimbaji huyo kutoka label ya PKP amesema msanii kuishi maisha ya namna hiyo ni kitu kibaya kwani anataka kuwaaminisha watu kuwa ndivyo alivyo wakati sivyo.

“Msanii mwingine anaweza akafanya hivyo kwa ajili ya kuonekana kwa watu kuwa ana muonekano fulani wakati hana, mwisho wa siku anapokuja...
kupokonywa kile kitu inakuwa imemuharibia kabisa” amesema Nedy Music.

“Ni maisha fulani mabaya huenda hata watu wanayatamani lakini siyo maisha mazuri kwa msanii kuwa hivyo, lakini kwa anayefanya hivyo siwezi kujua anayachukuliaje,” ameongeza.

Katia hatua nyingine msanii huyo amesema kolabo yake na msanii Mr. Blue imeshakamilika na muda wowote itatoka.

0 comments:

Post a Comment