Pages

Subscribe:

Tuesday, November 28, 2017

BEKA FLAVOUR: ASLAY HANA MSAADA WOWOTE KWANGU

Msanii Beka Flavour ambaye ni moja ya zao la Yamoto Band, amesema kwamba baada ya kundi hilo kusambaratika hapati msaada wowote kutoka kwa wenzake kama ilivyokuwa awali. 

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Beka amesema kwenye kazi zake za sasa msanii mwenzake Aslay hajamsaidia kitu chochote, na hata yeye hajampa...
msaada wowote Aslay kwani kila mtu anapamba ili kuweza kusimama.

“Sijawahi kumuandikia nyimbo Aslay na wala yeye hajawahi kuniandikia, wala hajawahi kunisadia chochote, kila mtu anapambana na hali yake, ila mtu akiwa na kazi mpya tunasikilizishana, jana Aslay kanisikilizisha ngoma zake mbili ambazo hazijatoka”, amesema Beka Flavour.

Hivi karibuni Beka Flavour ameachia kazi mpya ambayo inajulikana kwa jina la 'Sarafina' na kuwa msanii wa pili kutoka Yamoto Band kuachia kazi mara kwa mara wakiwa kama 'Solo Artist'.

0 comments:

Post a Comment