Pages

Subscribe:

Sunday, November 26, 2017

YANGA WAFANIKISHA MNASA KAYEMBE KANKU KTK USAJILI WA DILISHA DOGO


Klabu ya Yanga imefanikiwa kunasa saini ya beki wa kati, Fiston ‘Festo’ Kayembe Kanku kutoka klabu ya Balende FC ya DR Congo kwa  mkataba wa miaka miwili.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga iliyotolewa kupitiwa kurasa zao za mitandao ya kijamii  zimedai kuwa Kayembe alikuwepo nchini akifanya majaribio kwa muda mrefu chini ya...
kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina.

“Fiston ‘Festo’ Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mabingwa mara 27  Yanga akitokea Balende FC ya DR CONGO. Festo anayeimudu vyema nafasi ya mlinzi wa kati amefanikiwa kusaini kandarasi hiyo baada ya majuma kadhaa ya majaribio chini ya kocha George Lwandamina.”

Usajili wa Kayembe unakuja muda mfupi baada ya Yanga jana kuruhusu goli la tano kwenye ligi kuu msimu huu ambalo lilipelekea timu hiyo kulazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons kunako dimba la uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

0 comments:

Post a Comment