Pages

Subscribe:

Tuesday, November 21, 2017

BARAKAH THE PRINCE KUJA NA BANA MUSIC STUDIO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya cha Bongo Fleva kutoka Tanzania, Barakah The Prince ametangaza ujio wa kitu kingine ambacho ni kikubwa chini ya kivuli cha lebo ya muziki inayomhusu kwa ushirikiano wake na mpenzi wake Naj, BANA MUSIC.

Akipiga stori Barakah amesema kuwa ni kweli amekuwa akifanya kazi na watayarishaji na studio ambazo zinamhitaji na anazohitaji pia kulingana na ukaribu wao, lakini sasa wako katika...
umaliziaji wa studio za BANA na utaanza kuaandaa kazi muda wowote kuanzia sasa.
“Nimeamua sasa niliweke wazi kwasababu wengi wanaona nafanya kazi studio tofauti na wanajiuliza maswali, studio za BANA MUSIC iko katika umaliziaji na kazi soon itaanza. Kazi zenye ubora ni kikubwa tunachozingatia na naamini utayarishaji wetu unazingatia kile ambacho mashabiki wanahitaji kukisikia” Amesema Barakah The Prince.
Hata hivyo Barakah ameweka bayana kuwa mbali na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa lebo ya BANA, wapo wasimamizi ambalo wanaisimamia lebo hiyo na muziki wake kwa ujumla katika kuhakikisha kazi zamuziki wake zinaenda na lebo inaweka mizizi ya kusonga mbele.

0 comments:

Post a Comment