Pages

Subscribe:

Wednesday, November 22, 2017

CLOUDS FM YAPIGWA FAINI YA MILIONI 12 NA SERIKALI KWA MAKOSA HAYA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya mawasiliano ‘TCRA’ imeipiga faini Clouds FM Radio jumla ya shillingi za kitanzania milioni 12 kwa makosa matatu ya kimaaudhui na kanuni za utangazaji.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salam kuhusiana na maamuzi ya kamati ya maudhui, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Joseph Method Mapunda amesema kuwa kosa la kwanza la kituo hicho ni...
kukiuka kanuni na maudhui ya utangazaji, na kutangaza habari zisizo na ukweli(uongo) na za upotoshaji katika kipindi cha Jahazi cha saa 11 Jioni katika kipengele cha Mastori ya Town na kosa hilo imetozwa faini ya Sh. milioni 5.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Maudhui, Joseph Method Mapunda.

Katika hatua nyingine ya faini, Clouds Fm imetozwa Shilingi milioni 5 nyingine kwa kosa la ukiukaji wa kanuni katika kipengele cha ‘Najua Wajua’ huku kupitia kipindi cha XXL, Clouds Fm ikitozwa faini ya Sh. milioni 2 kwa kosa la ukiukaji wa kanuni za utangazaji pia.

Kutokana na makosa hayo matatu, Kituo hicho kimetozwa Jumla ya shilingi za kitanzania milioni 12 kwa makosa yote matatu na watatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku 30 kuanzia tarehe 21 Mwezi Novemba 2017.


Vile vile kamati hiyo ya maudhui imewapa onyo kali na imeaswa kuchukua hatua kali kwa watangazaji wanaokiuka maadili ya utangazaji ambapo faini hizo imeambatana na Clouds kutakiwa kuwaomba radhi wasikilizaji na wananchi ujumla kwa muda wa siku 3 mfululizo kuanzia siku ya jana(tarehe 21 Novemba 2017) katika kipindi cha Jahazi.

0 comments:

Post a Comment