Sunday, November 26, 2017
NYOTA NDOGO AWATETEA AKINAMAMA NCHINI KENYA KWA UJUMBE HUU
Muimbaji kutoka nchini Kenya, Mwanaisha Abdalla a.k.a Nyota Ndogo ameambatanisha ombi lake kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta anayetegemea kuhapishwa 26 mwezi Novemba mwaka huu.
Akiyatumia maneno yanayoashiria kuguswa na uchungu wa kile chenye sura ya unyanyasaji wa akinamama na jinsia ya jamii ya watoto wa kike kwa ujumla, Nyota Ndogo amemuomba Rais Uhuru Kenyatta...
kulitazama hilo kwa kuweka mikakati ya kuwawezesha wanawake kupewa haki zao hasa pindi wanapotekelezwa na wanaume wanaowatia mimba na kutelekezwa.
Kupitia Instagram account nyota ndogo ameandika:
Ujumbe wangu kwa rahisi wa jamuhuri ya kenya @president.of.kenya .bado siku tatu uwapishwe na kutuongoza wakenya tena kwa miaka mitano.#OMBILANGU. nakuomba uwaonee wanawake huruma na uwape kipao mbale maana ndio mama zetu dadazetu na bibi zetu sio?
NAOMBA UWEKE SHERIA YA MIMBA.WEKA SHERIA KUA MWANAMKE YEYOTE ATAKAEPATIKANA NI MJA MZITO BASI MWENYE MIMBA ILE NILAZIMA KUILEA ILE MIMBA NA KUMLEA YULE MTOTO MAANA NIWAKE AMA KIWANGO CHA MSHAHARA WAKE UENDE KWA MAMA MTOTO KWAAJILI YA KULEA HUYO MTOTO.WAUME WENGINE UWACHA WAKE ZAO WAKAENDA TIA MIMBA NJE AKAKUKIMBIA UKIMUULIZA ANAKWAMBIA NIPO NA MKE.KWAIVYO HUYU MTOTO MAMA ANAISHIA KUMLEA MWENYEWE KWASHIDA NA NDIO WENGINE USHINDWA WAKAISHIA KUTOA ZILE MIMBA.PLZ WEKA SHERIA HII TAFADHALI @uhurukenyatta itasaidia sana pia waume kujali plzz
#SHERIAKWAAJILIYAWANAWAKE...KAMA WEWE NI MWANAMKE NA UNANISAPOTI PLZZ TAG RAIS NA UTAG MTU UNAEFIKIRIA IKIMFIKIA ITAMFIKIRIA NA RAISI.KAMA NIDHAMBI TUMEFANYA PAMOJA KWANINI NIBEBE UKUMÙ PEKEANGU😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭..sio tabia yangu kutag watu but Leo nitawatag hawa watu muimu.
Hata hivyo katika hatua za uapishwaji, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli atakuwa miongoni mwa viongozi mbali mbali duniani watakaohudhuria kuapishwa kwa Rais huyo wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment