Pages

Subscribe:

Friday, November 24, 2017

RAPA SOLO THANG APATA MTOTO WA KIUME


Staa wa muziki wa Rap na mwanakikundi cha muziki wa rap cha WATEULE kutoka nchini Tanzania anayeishi Ireland, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang amapata mtoto wakume aliyepewa jina la ‘Zayn’.

Akipiga mastori, rapa Solo amethibitisha kilichoonekana katika ukurasa wa akaunti yake ya Instagram kuwa ni kweli amepata mtoto wa kiume ambapo kwa ujio wa mtoto huyo imekuwa baba mzazi wa watoto wa tano kwa...
hesabu ya ujumla wa watoto wake.

“Yeah tarehe 17 mwezi huu wa Novemba nimebahatika kupata mtoto wa kiume ambaye nimempa jina la Zayn, kwa hiyo kwa sasa anakuwa ni mtoto wa nne kwa huku nikanoishi na nina watoto wa kike wawili ambaye ni Yusria na Zaynab na wa kiume wawili ambao ni Yassir na Zayn” Amesema Solo Thang.

Hata hivyo kukamilisha idadi kamili ya watoto watoto wa tano, Staa huyo wa ngoma ya ‘Uchu’ ana mtoto wa kiume anayejulikana kwa jina la ‘Farees’ mtoto anayeishi nchini Tanzania.

0 comments:

Post a Comment