Sehemu ya:2
Mtunzi: Agatha Francis
"Sawa mume wangu sasa nimekuelewa sio unakua
muoga unadhani tukiacha mali itakuaje ila itakua vizuri sasa ukimpigia
simu kaka Mark pia aje maana peke yetu hatutoweza maana tangu aondoke
hajarudi kabisa", mke wa Baraka aliongea.
Basi walicheka sana Baraka
alimtania mke wake kwakusema mwanamke mbishi wewe ungekua mwanaume sijui
ingekuaje usijali lakini Mark nampigia sasa hivi kaniletee...
simu ipo
kitandani pale, mkewe aliingia ndani kuchukua simu, alipokua rudi
alisema simu yenyewe kuna mtu alipiga sijui nani?,
Baraka alichukua simu
kuangalia nani aliyekua amepiga, alishangaa sana kisha akasema ni
shemeji Mark, yaani tunamuwaza na yeye anatuwaza wakacheka kisha mke
wake akasema piga sasa, Baraka alianza bonyeza simu iliapige mara simu
iliita na alikua Mark na mazungumzo yalikua hivi,
Mark:hello
Baraka:habari yako shemeji
Mark:wazima huko jamani
Baraka:sisi wazima sijui huko shemeji
Mark:mimi pia mzima, naomba niongee na dada yangu hapo kama yupo karibu,
Baraka:sawa haina shida, dada yako yupo, alipomaliza alimuewekea simu mkewe masikioni ili aongee na kaka yake
Mke:kaka habari za siku
Mark:nzuri dada, maendeleo?
Mke:salama
kaka yangu, mbona kimya kingi jamani, mke wa Baraka alianza kulalamika
lakini kaka yake Mark alikatisha mazungumzo yale kwakusema"usijali dada
yangu kesho nakuja huko nataka nimlete wifi yako umuone, kwahiyo mapema
sana nitakua huko.
mmmh sawa kaka, mke wa Baraka ambaye ni dada wa Mark
aliguna, kaka yake alishtushwa kisha aliuliza mbona unaguna dada yangu
kuna nini? dada alicheka kisha akasema karibu sana kaka yangu, sisi
utatukuta tunawasubiri tu, tutaongea mengi ukifika, sawa kaka alikubali
kishingo upande waliagana na simu ilikatwa.
Baraka aliuliza vipi mke
wangu anasemaje shemeji yangu maana nimemkumbuka sana, mke wake
alijibu"yaani kaka eti anakuja na mwanamke utadhani huku kijijini hakuna
wanawake yaani wanawake wa mjini siwapendi kabisa mimi, Baraka
alishangaa kisha akasema"lakini mke wangu kwani wanawake wa mjini wana
nini?, mbona unamatatizo wewe, wenyewe wamependana ndiyo maana anamleta
kwako yaani unagubu kweli wewe kwani wewe kuna mtu alikuchagulia, nini
Endelea kuifuatilia sehemu ya 3
Click hapa unifollow instagram SmashJuanito
Tuesday, November 28, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment