Pages

Subscribe:

Tuesday, November 28, 2017

SERIKALI YATANGAZA KUNUNUA CONDOM NA KUZIGAWA BURE NCHI NZIMA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kununua kondomu zitakazosambazwa nchi nzima bure, kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamaila wakatiu wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu na kueleza kwamba kondomu hizo...
zitasambazwa bila malipo.

Akiendelea kuelezea suala hilo Dk. Rusibamaila amesema kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya sehemu za starehe kama baa, nyumba za kulala wageni, migodini na katika kumbi za burudani, lakini takwomu zinaonyesha licha ya kuwa na ufahamu wa faida ya condom, idadi ya wanaoutumia ni chache zaidi.

“Takwimu zinaonyesha kwamba 69% ya wanawake na 77% ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU, lakini ni 27% tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund, ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030.

0 comments:

Post a Comment