Pages

Subscribe:

Monday, November 20, 2017

CASSPER NYOVEST ATOA ONYO KWA MARAPA WANAO TUMIA BANGI


Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest amesema hajawahi 
kutumia madawa ya kulevya aina ya bangi katika maisha yake ili kuongeza ubunifu 
kwenye muziki wake huku akiwaonya marapper wadogo waachane na dhana hiyo.

Cassper amesema hayo baada ya mdau mmoja kuhoji kwenye mtandao wa Twitter kwa kusema kuwa “Kwa mara ya kwanza namuona rapper akiiongelea vibaya bangi alikuwa ni Cassper. Bado najiuliza huyu jamaa ni rapper kweli au...
anajua kughani tu?”
Ndipo Cassper akaona amjibu mdau huyo tena kwa kumshangaa kuwa haamini kwamba kila rapper mzuri ni lazima atumie bangi au aisifie kwani haina faida yoyote katika ubunifu kwenye muziki.

“Unaongelea nini? Yaani kuwa rapper ni lazima uvute bangi? au lazima niisifie ndiyo niwe rapper? Sawa, sivuti bangi wala kuifikiria kwa lolote. Na nashauri mtoto yeyote anayenitazama kutokuiga maisha yangu au kujaribu kuvuta bangi ili kuongeza ubunifu kwenye kazi yake kwani ni uongo tu.”ameandika Cassper Nyovest.

0 comments:

Post a Comment