Pages

Subscribe:

Sunday, November 26, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Kwanza) 01


Related image

Sehemu ya:1
Mwandishi: Agatha Francis

Hapana mke wangu sio vizuri kugombana na watu kwa hali hiyo uliyonayo, tumuache tu, MUNGU mwema tutapata sehemu ingine nzuri zaidi ya ile, ilikua ni sauti ya kijana Baraka akiongea na mkewe, "Hapana mume wangu, eneo lile ni mali ya wazazi wangu, walipofariki waliniachia linisaidie katika maisha, sasa yeye Mzee Moto la kwake tangu lini, mimi siwezi kumuachia mume wangu, kwahili utanisamehe tu", mke alimjibu.

Mume wake huku akionekana kakasirika sana lakini Baraka aliendelea kwakusema" mke wangu si unajua mzee Moto alivyo mkorofi kijiji kizima kinamtambua kwamba ni mkorofi na isitoshe mke wangu ni...
mjamzito wewe haipendezi kugombana katika hali hiyo", baraka alisema kwa upole ili mke wake amuelewe na kuachana na mzee Moto, hapana mume wangu mimi sitagombana nae, atagombana na sheria kwani ni lazima tufike muafaka siwezi kumuachia eneo lile hata kidogo ile hadhina yetu itusaidie katika maisha tena niliachiwa na wazazi.

Hapana mume wangu mimi lazima nipambane yeye na ukorofi wake kimpango wake ila sheria ifuate mkondo wake mimi siogopi chochote katika Mungu anajua tukifanyacho ni cha haki", aliongea mke wa Baraka kwa hudhuni sana, Baraka alimuonea huruma mke wake kwani ni kweli ilikua mali yake aliyoachiwa na wazazi wake lakini mzee Moto kwa tamaa zake anataka awapokonye. 

Baraka alimuangalia mke wake kwa hudhuni sana kisha akasema usijali mke wangu, mimi nitajitahidi ninunue eneo lingine ila tu usigombane na yule mzee, nakupenda sana mke wangu, lakini mzee yule anasifa chafu asije akatudhuru, mkewe alimtazama mume wake kisha alijibu kwa upole"nipo tayari kudhurika kwa kua ni mali ya wazazi wangu.

 Baraka au wewe huumii kwasababu sio ya wazazi wako"?, kauli ile ilimuumiza sana Baraka kwani ukweli ni kwamba alimpenda sana mke wake hivyo akutaka mke wake ajisikie vibaya hivyo akasema "hapana mke wangu, ulichonacho wewe ni changu pia na maumivu yako ni yangu pia ila nahofia tu usalama wetu, usinifikirie tofauti mke wangu, siwezi furahia maumivu yako, haina shida mke wangu tutaenda kwa mwenye kiti, kitakacho shauriwa ndicho, au unasemaje mke wangu",je mwenyekiti ataamua nini kuhusu mgogoro huo, usikose sehemu inayofuata😘😘😘😘😘😘😘

Click hapa unifollow instagram SmashJuanito

0 comments:

Post a Comment