Pages

Subscribe:

Wednesday, November 29, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Tatu) 03

Related image
sehemu ya:3 
Mtunzi: Agatha Francis

"mbona unagubu sana mke wangu jamani", alipofika hapo aliona sura ya mke wake ikibadilika na kwakua alimjua mke wake ni mkorofi ilibidi aanze kujichekesha akisema"mke wangu bhana, muache bwana shemeji achukue jiko ndiyo mda wake sasa", mke wake hakujibu jibu kwani maneno ya mume wake hakuyapenda.

Basi mambo muhimu ya nyumbani yalifanyika siku ile nakusubiri kesho ambayo Mark alihaidi atapeleka mke kwa dada yake. Siku ilipofika mkewe Baraka...
aliamka mapema kama ilivyokawaida yake, alifanya shughuli zote, siku hiyo aliamka kachangamka kwani hasira za jana zilimuisha na anampenda mume wake, walikunywa chai lakini muda ulienda sana mpaka majira ya saa7 Mark hakufika nyumbani kwa dada yake. 

Baraka akauliza, mke wangu, vipi shemeji amehairisha mbona hafiki?, mmmh hata mimi sijui kwakwel maana mda unazidi kwenda ata kwa mwenyekiti sijui tutaenda saa ngapi, kabla hajajibiwa swali lake na mumewe Baraka aliwaona kwa mbali Mark na binti mmoja wakiwa na baadhi ya mifuko. 

Basi Baraka alimuonesha mkewe ujio wa Mark, mkewe alipoona alifurahi sana, aliinuka na kwenda kumpokea kaka yake, walikumbatiana kwa furaha hali iliyomfanya Yule binti mgeni atambue upendo kati ya Mark na dada yake, hivyo aliishia kutabasamu tu, walikaribishwa mpaka eneo ambalo waliketi awali yeye na mumewe Baraka. 

Walipoketi eneo lile walisalimiana kipindi hicho mkewe Baraka akiwa karibu na kaka yake yaani Mark, baada ya mazungumzo ya hapa na pale Mark alianza kwa utumbulisho, jamani dada na shemeji yangu huyu mbele yenu anaitwa Nancy lakini jina maarufu sana ni mama Careen, alipofika hapo dada yake yaani mke wa Baraka akauliza kwakutahamaki akirudia jina lile maarufu"mama Careen, mmh kwani kaka unamtoto anaitwa Careen?

Mark alitabasamu kisha alijibu kwa uhakika zaidi "hapana dada yangu, ni Mtoto wa Nancy, hivyo ni mwanangu pia kwani Nancy alipozalishwa tu mumewe alikimbia, alipofika hapo akamtizama Nancy akitabasamu, dada yake ambaye ni mke wa Baraka alianza kucheka, alicheka sana kisha alipiga makofi akisema kwakweli kaka umechanganyikiwa, kwani wewe ndiye unayejua kuoa wanawake waliotelekezwa si ndiyo?😀😀

Tukutane sehemu ya 4

0 comments:

Post a Comment