Pages

Subscribe:

Thursday, November 30, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Nne) 04

Related image
sehemu ya:4
Mtunzi: Agatha Francis


Au wewe ndiye mtu unayejua kulea watoto wa wenzio kabla huzaa wa kwako, kaka yangu vipi wewe", Mke wa Baraka aliongea maneno yale kiasi kwamba mumewe na nduguye Mark walibaki wakishangaa, mama Careen machozi yalimtoka tu hakuweza ongea chochote kile lakini mkewe Baraka hakujali yote hayo aliendelea.


"samahani mama Careen, kaka yangu najua ananiheshimu na kunisikiliza hawezi kuoa mwanamke ambaye tayari umezaa vipi mumeo akirudi si na wewe...
utamuacha kaka yangu, mimi sitaki kwakweli, halafu kaka Mark, wewe huku kijijini kuna Suzan vipi tena?, ushakwenda mjini basi umevurugwa mwenyewe".

Alipofika hapo Baraka alishindwa vumilia akasema"mke wangu, wageni ndiyo kwanza wamefika jamani bora ata ungeongea masuala ya kwa Mwenyekiti jamani, tabia gani hiyo mbele ya mgeni, huku akimtazama mama Careen kwa huruma", Mark alishindwa vumilia maneno ya dada yake aliinuka na kumshika mkono dada yake na kuwaacha mama Careen na Baraka.

Mama Careen aliendelea kulia kisha akasema"kaka yangu nakushukuru kwa moyo wako wa ukarimu, ila kama ningejua Mark anamchumba tayari mimi nisingekuja mpaka huku, naamini ananipenda lakini hakuna ndoa mbaya kama ndugu hawajakukubali, acha mimi niondoke utaniagia Mark", alipofika hapo alifuta machozi yake nakuinuka pale alipokua ameketi, Baraka alishindwa sema chochote kwani hakupenda maneno ya mke wake, alikasirika sana, alibaki ameketi akiwa haelewi chakufanya. 

Mark alipokwenda na dada yake ndani aliongea kwakutumia, "dada, nini unafanya?unajua yule mwanamke nmemkuta wapi?mwanake mtiifu, mwanamke ananipenda kwa dhati leo unamdharirisha kiasi kile, unadhani mimi nitamjibu nini sasa eee, unadhani mimi ntafanyaje?, Mark alishindwa zuia machozi Yake alijikuta akilia, dada yake akasema kaka wanawake wa mjini huwajui wewe umesahau wazazi walikuambia mkeo ni Suzan, sasa kazi kwako mimi sitasema lolote ila utakapokua unaondoka huku kijijini utaondoka na Suzan sijui huyo mama Careen wako utamuweka wapi.

Mimi kama dada yako nimemaliza, jiandae twende kwa mwenyekiti maana unanichanganya tu kila kitu utajua hukohuko sawa", alimaliza kisha alitoka nje.
Alipofika nje aliuliza, huyo wifi mama kaenda wapi?,


Usikose Sehemu 5
Click hapa unifollow instagram SmashJuanito

0 comments:

Post a Comment