Pages

Subscribe:

Wednesday, November 22, 2017

JACAN AKABANA KOO NA WANAO SIMAMIA KAZI ZAKE ZA MUZIKI

Rapa kutoka Tanzania na mkali wa ngoma ya ‘Control’ iliyomshirikisha Muimbaji Nova chini ya usimamizi wa Kissmusic Entertainmet, Jacan amenekana kukinzana na uongozi wake kwa madai ya kucheleweshwa kwa kazi yake mpya.

Kupitia jumbe picha za mazungumzo yake na Uongozi wake huo(Screen Shot), Jacan alionekana kubishana kwa majibizano tofauti ya sms akionesha kutokubaiana na uongozi kiasi cha uongozi wa menejimenti yake kutishia...
kufikishana pabaya endapo kazi yake mpya itatoka katika muda ulio nje ya makubaliano ya mkataba.
Hata hivyo ilionekana wazi kuwa picha za jumbe hizo za mabishano zilionekana kuwa zimesambaa kutoka upande wa uongozi ambapo jitihada za kumtafuta Jacan zinaendelea ili kujua hatma na nini kitafuata baada ya uongozi kudinda kuachia kazi ambayo tayari imeshakamilika.

Vile vile Jacan chini ya uongozi huo wa ‘Kissmusic Entertainment’ wamefanikiwa kuachia kazi moja tu ya ‘Control’ hivyo ujio wa pili kabla kuingiza kazi sokoni yakaibuka marumbano.

0 comments:

Post a Comment