Pages

Subscribe:

Saturday, December 23, 2017

HIZI HAPA NJIA BORA ZA ASILI JINSI YA KUKUZA NYWELE

Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair, tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.
Je,unazifahamu nywele zako vizuri? Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini?
1.Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda. Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga ... mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.
2.Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.
3.Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji. Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu. Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.
4.Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje?
Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.
Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.
Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.
(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.
Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.
Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya uvuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.
5.Mafuta ya Kupaka kichwani.
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele  aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya Zaituni Olive(extra virgin) na ya Tea tree.
6.Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana.sio kitana.Chanuo kubwa(wide toothed comb).
7.Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka.Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.
8.Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi.Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24.
Kwa leo naishia hapa.Tukutane tena wakati ujao kwenye kujuzana zaidi.Unakaribishwa kwa maoni,ushauri na kupendekeza mada yoyote izungumziwe kuhusu nywele asilia.
Mada ijayo tutazungumzia aina za nywele zilizopo humu duniani kwa ujumla.
Nakutakia mapenzi mema ya nywele zako,natumaini mmefahamiana kiasi sasa.

0 comments:

Post a Comment