Pages

Subscribe:

Sunday, December 31, 2017

MBAO FC YAVIMBA YAONESHA UKOMAVU KWA YANGA SC



Klabu ya Yanga imefunga mwaka 2017 kwa kipigo kitakatifu kutoka kwa klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kwenye mchezo wa mzunguuko wa 12 wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

Kipigo hicho cha magoli mawili nunge kimewafanya Yanga washuke hadi nafasi ya nne kutoka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mahasimu wao...
Simba SC ndio vinara mpaka sasa. Tazama msimamo kamili wa VPL

Magoli yote ya Mbao FC yamefungwa na Habib Kiyombo kunako dakika ya 53 na 68 ya mchezo huo uliyokuwa na msisimko wa hali ya juu.

Mchezo mwingine uliopigwa leo ni kati ya Njombe Mji na Singida United ambapo Singida wameibuka na ushindi wa goli 3-1 kunako dimba la Sabasaba mjini Njombe.

0 comments:

Post a Comment