Pages

Subscribe:

Saturday, December 23, 2017

BARAKAH THE PRINCE AMKATAA MTOTO ANAE SEMEKANA KAZAA NA VIDEO QUEEN

Msanii Baraka The Prince amekanusha kuzaa mtoto na video queen Careen ambaye ni mkazi wa Arusha, kama ambavyo imesambaa mitandaoni. Akifanya mahojiano na kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kwamba hajazaa na binti huyo na wala hajawahi kukutana naye kimwili.

Licha ya kuchezwa sauti ya binti huyo ikiongolea kuwa Baraka ndiye baba wa mtoto huyo, amesema ingawa mama mtoto kasema ni wake lakini sio kauli ya kuamini kwani ameshapitia...
mambo kama hayo.

“Nina mtoto mmoja yuko Arusha, mama anaitwa Farida, ni mtoto wangu, hizo stori zingine sio kweli”, amesema Baraka The Prince.

Pamoja na hayo Baraka amekanusha taarifa za kuachana na mpenzi wake, na kusema kwamba bado wapo pamoja.

0 comments:

Post a Comment