Pages

Subscribe:

Saturday, December 23, 2017

LULU DIVA: SIJAUMIA BELLE 9 KUFUNGA NDOA WALA SINA KINYONGO

Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa- Lulu Diva
Msanii anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuweka wazi hisia zake kwamba anamzimikia msanii mwenzake, Abednego Damian ‘Belle 9’ ambaye amefunga ndoa ya siri siku chache zilizopita amesema kuwa, hana kinyongo na wala hajaumia na jambo hilo
Akizungumza baada ya kuenea minong’ono ya wambea wa jiji kwamba kitendo cha Belle 9 kufunga ndoa kitakuwa kimemuumiza mrembo huyo alisema, hajaumia hata kidogo sababu kwa sasa...

Belle 9 ni rafiki yake wa karibu wala hawazi tena mambo ya mapenzi.
“Ni kweli niliwahi kuweka wazi hisia zangu kwamba namzimikia enzi hizo, lakini hayo yalipita Belle 9 tunaheshimiana kama marafiki tu, pia nashukuru alinialika kwenye harusi yake lakini mambo yalinibana nikashindwa kwenda, kikubwa nampongeza kufunga pingu za maisha,”alisema.

0 comments:

Post a Comment