Pages

Subscribe:

Friday, December 22, 2017

ROSTAM KUVUNJIKA KABLA YA MWEZI HUU KUISHA

Umoja Wa Roma Na Stamina Kuvunjika Kabla ya Mwakani
Wasanii wawili waliokuwa wakiunda kundi la Rostam (Roma na Stamina), ambao wameanza kufanya vizuri kabisa katika muziki huku sasa hivi waki-hit na kibao chao chao cha kiba100 wanaweza kuvunjika na kutokufanya kazi tena pamoja kutokana na wawili hao kuwa  na upishani sana hasa kwenye swala la ratiba.

Akiongea na chombo kimoja cha habari , mmoja wa wanaunda kundi hilo anaefahamika kama Roma amesema kuwa wamekuwa wakipishana sana na mwenzie Stamina kutoakana na...
kuwa busy sana na hata kuna muda wanashindwa kufanya baadhi ya mahojiano muhimu katika radio stations kwa sababu ya safari zake zisizokuwa na msingi.

Roma anasema kuwa Stamina amekuwa ni mtu wa kupoteza ratiba nyingi sana hasa kutokana na kuangalia mpira muda mrefu huku yeye hawezi kufanya kitu kama hicho, hata hivyo roma anasema kuwa kuna kipindi wanaweza kukwaruzana akatamani hata kumpiga vibao kutokana  na kumpotezea madili yake mengi.

Roma anaendelea kusema kuwa kuna wakati alipigiwa simu anahitajika katika interview lakini mwenzie alipomjulisha alimjibu yuko njiani anakwenda mMrogoro ilhali yeye hakuwa na taarifa hizo wakati wapo katika muunganiko wa kikazi.hata hivyo msanii huyo alio ngea katika kipindi cha now you know kwamba hajui kama kundi ili litaweza kutoboza mwezi desemba na kuvuka mwaka kabla halijavunjika.

Roma na Stamina walianza kufanya kazi pamoja mwaka huu, wakiamua kuunda kundi hili kutokana na aina ya muziki wanaofanya kuendana lakini upishani wao unakuja pale ambapo kila mmoja anakuwa na interest tofauti.

0 comments:

Post a Comment