Pages

Subscribe:

Sunday, December 24, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 11) - 11

Related image
Sehemu ya:11 
Mtunzi: Agatha Francis 

Basi Mark alifika nyumbani na kumkuta Suzy akiwa bado kakaa sebuleni kwani hata chumbani hakuoneshwa, Mark alipofika alipitiliza chumbani na kujitupa kitandani na Suzy naye alifuata chumbani na kujilaza kitandani. 

Mark alianza rasmi maisha na mwanamke Yule siku hiyo na Suzy alijitahidi kua mnyenyekevu kwa Mark kiasi kwamba Mark alianza...
kumzoea Suzy. Kijijini maisha yaliendelea dada yake Mark yaani mke wa Baraka sasa alibakiza siku chache ajifungue. Mume wake Baraka alijitahidi kufanya shughuli za nyumbani ili mke wake ajifungue salama. 

Ndipo siku moja usiku majira ya saa 2 hali ya mke wake haikua nzuri sana hivyo alimpeleka hospitalini walipokelewa vizuri sana na mhudumu aliyekuwepo muda ule, mke wake hakua na hali nzuri kabisa alibanwa sana, Baraka alichanganyikiwa sana kuona ile hali ya mke wake lakini mhudumu yule alimuhakikishia kwamba atajifungua salama na wala asiwe na hofu zaidi amuombee tu kwani inaonekana kujifungua muda si mrefu, mhudumu Yule yaani Yule nesi alimuhudumia mke wa Baraka vizuri mpaka majira ya usiku sana alijifungua mtoto wa kike.

Lakini mtoto Yule hakua na afya kama watoto wengine na alipompima uzito alikua na 1.5kg hali hiyo aliogopa sana Yule kwani mtoto mwenye afya ni 2.5kg sasa huyo mtoto itakuaje, basi alitoka na kumkuta Baraka amelala nje, alipofika alimuamsha na kumweleza hali hali halisi, Baraka aliogopa sana lakini Yule nesi alisema "kama mtafuata maelekezo mtoto huyo atakua vizuri tu wala msijali kwani wengi huzaliwa na hali kama hizo", 

Baraka kidogo alimuelewa mhudumu nakusema asante sana dada angu ubarikiwe, vipi lakini ninaweza kwenda kumuona?, basi aliruhusiwa kisha Baraka alielekea kumuona mke wake, alipofika chumbani kwa mke wake alikuta tayari kalala kwani alikua amechoka sana, yeye pia hakutaka kumsumbua mke wake hivyo akalala kwenye kiti kilichokuwepo mule ndani mpaka asubuhi, basi walipoamka alimsalimia mke wake na kumpa hongera kwani mpaka Muda huo mke wake hakupewa taarifa kuhusu mwanae basi Baraka alitoka na kwenda kumtafutia chakula mke wake. 

Aliporudi mke wake alikula akamaliza na mara nesi aliingia chumbani na kumwambia hongera sana dada vipi umemnyonyesha mtoto?, 

usikose 12

0 comments:

Post a Comment