Pages

Subscribe:

Friday, December 22, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Tisa) 09

Related image
Sehemu ya:9
Mtunzi: Agatha Francis

Suzy aliguna kisha akasema"kaka yako kasema ata kama akinipenda akanioa ana mwanamke mwingine ambaye anampenda sana, sasa sijui itakuaje, mke wa Baraka akasema usijali wifi yangu, huyo mwanamke mwenyewe wa mjini ana mtoto hawezi kumuoa buana cha msingi hapa wewe jitahidi tu kumpenda nina imani atakupenda tu sawa. 

Suzy alifurahi sana kusikia hivyo akasema nakushukuru sana wifi yangu jamani nitafurahi, nitampenda Mark siunajua ninavyompenda, basi walicheka sana, lakini Suzy alijisemea moyoni"pole sana wifi yangu yaani...
mimi nikiingia ndani ya nyumba ya ndugu yako nina imani hautocheka na mimi tena wala ata kunipenda tena. Basi mke wa Baraka aliomba Suzy akajiandae tu kesho yake ataondoka na Mark basi waliagana na Suzy aliondoka kurudi nyumbani kwao. 

Suzy yeye aliishi peke yake kwani wazazi wake walifariki zamani sana, hivyo aliishi peke yake hakua na ndugu wa karibu sana kwake kwahiyo alifurahia sana kwenda kuishi na Mark kwani Mark alikua kijana mfanya biashara hivyo aliamini ataenda kuchuma mali nyingi ili abadilishe mfumo wa maisha yake. Mark hakuongea chochote siku ile alisubiri siku inayofuata ili aondoke kijijini maana mambo ya dada yake hayakumpendeza. Basi ikawa usiku ikawa asubuhi.

Suzy alikua tayari kafika kabla hata watu hawajaamka, alikaa nje akisubiri waamke, mke wa Baraka alikua wa kwanza kuamka alishangaa sana kumkuta Suzy pale nje, alimtania kwakusema "wifi wewe ni kiboko kwakweli ndiyo umemuwahi mume hivyo basi wote walicheka Suzy akajibu kwakucheka yaani ndugu yangu usingizi uligoma, maana nilihisi Mark ataondoka maana ndoa za siku hizi hahahhahah walicheka sana,.

Baada ya muda kidogo wote Mark na Baraka waliamka, walishangaa sana kumkuta Suzy pale akiwa na nguo zake, Mark alibanwa na kicheko kwani jambo hilo lilimshangaza sana, Baraka alilitambua hilo alimvutia ndani alianza kucheka na kusema shemu unamcheka mkeo acha bhana, Baraka akasema "usione nacheka shemu yani mambo ya ajabu haya kweli dada kaniletea mke kwa lazima sitaki amini ila ndio ukweli wenyewe sijui nitafanyaje sasa, Baraka alimuambia shemeji yake ondoka naye ukiona hafai achana naye kwani sio lazima shemeji yangu, sawa,Mark alijibu usikose 10.

0 comments:

Post a Comment