Pages

Subscribe:

Friday, December 29, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 14) - 14

Related image
Sehemu ya 14 
Mimi nina hakika mtoto mzima kabisa", alimbembeleza mke wake, waliendelea kubembelezana mpaka asubuhi ilipofika, Baraka alikua wa kwanza kuamka ili kufanya mawasiliano na Mark na kumueleza kuwa wanaenda mjini. 

Mark aliwakaribisha sana kisha mama Prisca aliamka na safari ilianza, walipanda gari na kuelekea mjini, haikuchukua masaa mengi wakawa wamefika mjini, Mark alifika stendi kuwapokea na...
kuwapeleka nyumbani. Walipofika nyumbani walikaribishwa mpaka sebuleni, mama Prisca alimuulizia wifi yake.

Mark alijibu kwamba yupo chumbani, mama Prisca alihoji tena kwani hajui kama leo tunakuja kwenu?, Mark alijibu nilimwambia lakini sijui kwanini hatoki chumbani, mama Prisca aliita "wifi, wifi we Suzy, "Suzy alijibu "unasemaje" Mark aliguna na kumuangalia Baraka, Baraka alishangaa na kumuangalia mke wake, mama Prisca hakukubali akasema"nasemaje mimi, au hujajua unaitwa na nani?", Suzy akiwa chumbani akajibu "nakuja bhana"hali ya majibu yale iliwashangaza Baraka na mke wake lakini Mark aliona kawaida tu. 

Basi Suzy alifika sebuleni aliketi na kusema"karibuni"yaani kama watu ambao hajawahi kuwaona, watu walibaki wakishangaa, Mark akasema"vipi Suzy, ushawaandalia wageni chakula nilichokuagiza", Suzy bila wasiwasi akasema "hapana maana nilijisikia kuchoka hivyo nikaingia kulala lakini wifi jiko lile pale unaeza kwenda kupika kisha aliinuka nakurudi chumbani, hali ile ilimtia hasira mama Prisca akajikuta akisema ina maana kaka hua humpigi mkeo si ndiyo, ndiyo maana anakudharau, 

Mark akajibu"wala hanidharau mke wangu ananipenda sana wewe si ndiye mwanamke uliyempenda huyu sasa utakiona cha moto wewe tulia tu", Baraka akacheka sana akasema duuuu umdhaniae ndiye kumbe siye mbona balaa hili, mda wote mama Prisca aliinamisha kichwa chini kwa aibu basi Mark aliinuka na kwenda tafuta chakula kwa ajili ya wageni wake. 

 Usiku ulipofika Suzy alianza kupika alipomaliza alimpakulia mume wake kisha kilichobaki katika sufuria tena bila mboga alimpa wifi na mume wake yaani Baraka, Baraka alikasirika sana hakula chakula kile, mama Prisca akasema"Suzy nini hiki?", Suzy alijibu maisha ya mjini mipango wifi yangu we kula tu kwani tatizo nini?

usikose sehemu ya 15

0 comments:

Post a Comment