Pages

Subscribe:

Saturday, December 30, 2017

SHILOLE: NATAMANI NA MIMI SIKU MOJA NIFANYE KAZI NA NICKI MINAJ


Msanii wa Bongo Fleva, Shilole amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva kwa sasa unakua kwa kasi duniani na kuufanya muziki huo kubadilisha maisha ya Wasanii huku akimtaja Diamond Platnumz kama moja ya wasanii wanaopambana kukuza muziki huo.

Shilole amesema “Bongo Fleva inaenda mbali sana, hususani! tuseme ukweli Diamond anaipushi sana Bongo Fleva yetu, sikutegemea kama  Diamond siku moja atafanya ngoma na...
Rick Ross sijui na akina Ne-Yo nilikuwa nikiona tuu tutafika huku? lakini tumeanza kujaribu na tunafika..Natamani na mimi siku moja nifanye kazi na Nicki Minaj.“amesema Shilole kwenye mahojiano yake na BBC Swahili.

Shilole ambaye yupo nchini Uingereza alikoenda kutumbuiza kwenye show maalumu amesema kuwa show za nje ya nchi siku hizi zinalipa tofauti na zamani.

0 comments:

Post a Comment