Pages

Subscribe:

Sunday, December 31, 2017

RAIS MSTAAFU AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA

Rais aliyeondolewa madarakani Jana December 30, 2017 amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kuvivunjia heshima vyombo vya mahakama.

Muhammad Mursi aliyekuwa Rais wa Misri amehukumiwa hukumu hiyo jana ikiwa bado anaendelea kuzuiliwa katika jela za nchi hiyo huku akiwa tayari amekwisha hukumiwa mara kadhaa ikiwemo kifungo cha...
maisha. 

Mbali na Muhammad Mursi, mahakama ya Misri pia imewahukumu watu 18 wengine kwa tuhuma hiyohiyo ya kuivunjia heshima  mahakama. Aidha mahakama ya Misri imemtaka Mursi kulipa faini ya Pauni milioni moja za Misri kwa jaji Muhammad al-Nemr.


0 comments:

Post a Comment